August 29, 2017


Nafasi ya Argentina katika kuwania kucheza Kombe la Dunia haijakaa vizuri na inalazimika kufanya kazi ya ziada kushinda mechi ijayo dhidi ya Uruguay.

Tayari kikosi cha Jorge Sampaoli kimeanza mazoezi na nahodha Lionel Messi na nyota kadhaa, wanaonekana kuwa makini wakitaka kushinda dhidi ya Uruguay ambayo wanaonekana kuchuana nayo.

Mazoezi yameanza katika jiji kubwa zaidi la Buenos Aires kwa ajili ya mechi hiyo na staa wengine ni kama Sergio Aguero, Mauro Icardi, Paulo Dybala na Angel di Maria.


Argentina ina pointi 22 wakati Uruguay ina 23, kila mmoja hana hali nzuri sana na anaonekana "kupigania hali yake".










0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic