August 18, 2017


Wakati Ligi Kuu Ujerumani, Bundesliga inaanza leo rasmi kwa kuwakutanisha mabingwa Bayern Munich dhidi ya Bayer Leverkusen kampuni ya StarTimes, imeandaa utaratibu wa kulipia hadi kwa Sh 1,000 tu.

Mkuu wa Masoko wa StarTimes, Juma Suluhu maarufu kama Sharobaro amesema mteja wao anaweza kulipia hadi Sh 1,000 (elfu moja) ambayo itakuwezesha kuona mechi moja au mbili.

“Hii itamfanya mtu akiamua kuona mechi za Bundelisga na nyingine kama Serie A kwa kulipia Sh elfu moja tu.

“Hata hivyo tunawashawishi wateja kulipia zaidi kwa kuwa kila unapolipa kwa muda mrefu bei inapungua zaidi,” alisema.

StarTimes ni pekee wanaoonyesha Bindesliga, Ligi ya Ujerumani ambayo inaongoza kwa kuwa na takwimu bora uwanjani na pia kuwa na timu inayoongoza kwa kuingiza mashabiki wengi zaidi uwanjani kila msimu.

Borussia Dortmund ndiyo inayoongoza kwa kuingiza mashabiki wengi zaidi kwa msimu uliopita ikifuatiwa na Barcelona, Manchester United, Real Madrid na Bayern Munich inashika nafasi ya tano na kukamilisha tano bora. 
















0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic