August 17, 2017

AJIBU (KATIKATI) AKIWA NA MAZOEZINI PAMOJA ANDREW VICENT "DANTE" NA RAPHAEL DAUD.


Ibrahim Ajibu ameifungia Yanga bao pekee wakati ikishinda bao 1-0 dhidi ya Chipukizi ya mjini Pemba.


Ushindi huo unamfanya Ajibu taratibu kuzima mjadala wa kwamba amekuwa hafanyi vizuri tokea ajiunge na Yanga.


Ajibu amefunga takribani mechi tatu za kirafiki lakini bado baadhi ya mashabiki wamekuwa wakionekana kutoridhishwa naye na kuzua mjadala kuhusiana na msaada wake.

Hata hivyo mwendelezo wake wa kufunga ikiwemo kufunga bao pekee dhidi ya Chipukizi Yanga ikijiandaa kucheza na Simba wiki ijayo, imeibua imani zaidi na kuzima mjadala.

Katika mitandao mbalimbali, hakukuwa na mjadala mwingine wowote tena kwamba hana msaada au ni kati ya wachezaji walioshindwa kuonyesha uwezo au wasio na msaada.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic