August 18, 2017




Kama ni mpenda soka ni lazima utakuwa unavutiwa na shabiki wa zamani wa Yanga, Ally Yanga kutokana na ushabiki wake kila timu yake ilipocheza.

Yanga ilimpoteza shabiki wake maarufu, Ally Mohamed ‘Ally Yanga’ ambaye alifariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea Mpwapwa, Dodoma.

Lakini kunaweza kuwa na faraja mpya kwa mashabiki wa Yanga baada ya mrithi wa Ally Yanga kupatikana/

Shabiki huyo mpya ambaye ameamua kwenda na ule mfumo wa marehemu Ally Yanga katika ushangiliaji, anaitwa Mack.

Mack ameanza kuonekana kwenye Uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam wakati Yanga ilipoivaa Ruvu Shooting na kupoteza kwa bao 1-0.


“Nilikuwa shabiki mkubwa sana wa Ally Yanga na baada ya kifo chake niliumia sana, kwa hiyo ili kumuenzi basi bora niige aina yake ya ushangiliaji wake kama kumuenzi,” alisema.

Mack alionekana kuwashitua baadhi ya mashabiki uwanjani pale kwa kuwa hawakuamini kumuona hadi walipoelezwa kwamba huyo ni shabiki mwingine.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic