Pamoja na kuibuka na ushindi, kocha msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, amekiri kuwa wapinzani wao wana timu nzuri ambayo ina uwezo wa kufanya vizuri kutokana na upinzani waliouonyesha katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliopigwa juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Simba iliibuka na ushindi wa penalti 5-4 katika mchezo huo baada ya matokeo ya 0-0.
“Tunashukuru tumeweza kuibuka na ushindi katika mchezo huu wa Ngao ya Jamii kwa sababu ndiyo kiashiria cha ligi kuanza na jambo zuri kwetu kuwa tumeweza kutwaa ngao yenyewe, naamini itatoa mwanga mkubwa kwetu katika msimu huu.
“Lakini kwa upande wa Yanga kiukweli walicheza vizuri, pengine walistahili kuibuka washindi isipokuwa penalti hazina mwenyewe, Yanga nimewaona niseme tu kwamba wana timu nzuri na yenye ushindani, naamini kama watajipanga vizuri watafika mbali katika ligi ya msimu huu kwa sababu waliweza kutibua vyema mipango yetu yote na kutupa wakati mgumu,” alisema Mayanja.
SOURCE: CHAMPIONI
SOURCE: CHAMPIONI
Uzalendo wa hali ya juu sana, hongera Mayanja
ReplyDeleteThe right words from the right coach. Big up Mayanja, you have done the truth.
ReplyDelete