August 6, 2017
PSG imeingiza kitita cha euro milioni moja siku ya kwanza tu ya mauzo ya jezi za Neymar.
Jezi za Neymar zaidi ya 10,000 zimeuzwa katika maduka mbalimbali ya PSG na kuingiza kitita hicho cha euro milioni moja (takribani Sh bilioni 2.6).
Inatarajiwa PSG kuendelea kuingiza mamilioniya fedha kupitia jezi namba 10 ya Neymar ikiwa ni siku chache tokea asajiliwe akitokea Barcelona.
Neymar ndiye mchezaji ghali zaidi baada ya kusajiliwa kwa mkataba wa miaka mitano uliogharimu kitita cha pauni milioni 198.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV