August 19, 2017




Zaidi Mohammed, Zanzibar
Simba imeitwanga Gulioni ya Unguja kwa mabao 6-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, mjini hapa.

Simba ikiwa bila mshambuliaji wake Emmanuel Okwi wala beki Juuko Murshid iliibuka na ushindi huo mnono ukiwa wa kwanza katika mechi zake za kirafiki.

Laudit Mavugo alikuwa wa kwanza kuwainua Simba katika dakika ya 13 na Shiza Kichuya akaongeza bao jingine dakika ya 37.

Mavugo ambaye alionekana ni moto, alifunga bao lake la pili likiwa la tatu la Simba katika dakika ya 40 na Juma Liuzio akaongez ana nne na Simba ikaenda mapumziko na mabao 4-0.


Kipindi cha pili angalau Gulioni walionekana kuchangamka na kutoa upinzani mkali kwa Simba lakini dakika ya 70, Mohamed Ibrahim maarufu kama Mo, akafunga la tano na kuhitimisha ushindi huo wa Simba wa mabao 5-0.

4 COMMENTS:

  1. Ndani ya habari kuna magoli sita! sasa ni matano au sita? na hili limekuwa likijirudia katika makosa ya kiuandishi mara kwa mara kwanini msiwe mnatulia kabla ya kutuma taarifa katika hii blog yetu pendwa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahaha kweli anynoumous.watulie kwanza kabla ya Kuandika hbr yoote....

      Delete
    2. Saleh anajitahidi saaana kwa waandishi makini ila kaka yangu namuomba awe anarudia ili kuondoa makosa ya kibinadamu@saleh jembe

      Delete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic