Real Madrid wameiangushia Barcelona kipigo cha pili, safari hii ikiwa ni mabao 2-0 na kufanikiwa kubeba ubingwa wa Spanish Super Cup.
Madrid iliitwanga Barcelona kwa mabao 3-1 nyumbani kwao Camp Nou, Barcelona.
Leo bila ya mshambuliaji wake, Cristiano Ronaldo aliyelambwa kadi nyekundu katika mechi ya kwanza, Madrid imeshinda kwa idadi hiyo ikiwa nyumbani Santiago Bernabeu.
Marco Asensio alikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya nne tu ya mchezo na Karim Benzema akapachika la pili dakika ya 39 baada ya kumuibia mpira beki Samuel Umtiti wa Barcelona.
Madrid imechukua ubingwa ikiwa na jumla ya mabao 5-1 baada ya ushindi wa mabao 3-1 ugenini Camp Nou.
That is Madrid we know!! Barcelona is as now as dog with no teeth.
ReplyDelete