Beki wa kati wa Yanga na nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ameweka wazi kuwa kama siyo bahati waliyokuwa nayo wapinzani wao, Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, basi wasingepoteza mchezo huo.
Cannavaro ambaye alikuwa jukwaani kwenye mchezo huo, aliwashuhudia wenzake wa Yanga wakipoteza mbele ya Simba kwa kukubali kufungwa penalti 4-5, kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar.
“Nikwambie tu hawa Simba wametufunga kwa sababu wamekuwa na bahati pekee lakini siyo suala la uwezo wa uwanjani kwani kama kiuwezo tumewaonyesha uwezo mkubwa tofauti na hata wengi walivyokuwa wanafikiria kwamba tungepoteza pambano hili kwa tofauti ya mabao mengi.
“Lakini sasa mechi imeshaisha na matokeo hayo tumeachana nayo, kikubwa tunaangalia kile ambacho kipo mbele yetu kuhakikisha kwamba tunatetea ubingwa pamoja na kuchukua mataji mengine,” alisema Cannavaro baada ya mchezo huo.
Cannavaro muda umefika wa kutundika daluga
ReplyDelete