August 20, 2017




Klabu ya Yanga imesema haina tatizo la viungo hata kama kiungo wake Papy Tshishimbi hatacheza katika mechi dhidi ya watani wao Simba.

Yanga itawavaa Simba katika mechi ya Ngao ya Jamii, Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesema wako vizuri hata kama hatacheza.

"Kama hatacheza tutasubiri hadi atakapokuwa fiti. Yanga haina tatizo la kiungo au viungo.

"Tuna viungo kama sita, hatuwezi kuwa na shida. Hivyo tuwaondoe wasi mashabiki," alisema.

Mashabiki wamekuwa na hamu ya kumuona raia huyo wa DR Congo akicheza mara tu baada ya kujiunga na Yanga huko Pemba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic