September 30, 2017




WAANDISHI WA GAZETI LA CHAMPIONI WAKIZUIWA KUINGIA MAZOEZINI.

Lile sakata la Obrey Chirwa kumpiga mwandishi Francis Dande wa Mtanzania limechukua sura mpya baada ya Yanga kukataa kufanya kazi na waandishi wote nchini.

Yanga ilikuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na waandishi wote walizuiwa kuingia kushuhudia mazoezi au kuwahoji waandishi.

Uongozi wa Yanga umechukua uamuzi huo siku moja tu baada ya Dande na Chirwa kupatanishwa na Kocha George Lwandanina.

BAADA YA KUZUIWA KUINGIA MAZOEZINI, WAANDISHI WA TBC WAKIWA NJE YA UWANJA WAKIJARIBU KUPATA PICHA.

Chirwa alianza purukushani hizo baada ya kupigwa picha alipoamua kubadilisha nguo katika eneo la uwanja,

Jambo hilo lilimkera akadai hawezi kupigwa picha akiwa nje ya uwanja ingawa hakuwa akijua sheria ya upigaji picha inaeleza vipi.

Kutokana na sakata hilo, Yanga imeamua kuvunja urafiki na waandishi wote wakiwemo wa vyombo vyote vya habari kwa kuwazuia kwenda mazoezini.

Jana, waandishi walizuiwa kuingia mazoezini bila ya maelezo huku baadhi ya wapambe wa baadhi wa viingozi wa klabu hiyo wakisimama getini kuwazuia waandishi.

Baadhi ya waandishi walilazimika kupiga picha kupitia baadhi ya upenyo wa uwanja huo huku wakilalama kwamba Chirwa pekee si Yanga na kama ugomvi haukuwahusu wao na wamekuwa wakifanya kazi kwa uelewano na klabu hiyo kwa muda mrefu bila ya bugudha.

Hata hivyo, waliokuwa eneo hilo walionekana kushikilia uamuzi huo ambao unaonyesha wazi hawajui maana ya vyombo vya habari na klabu za soka au uhusiano unaohimizwa na huenda wangeweza kulimaliza suala hilo bila ya kutengeneza chuki, uadui na waandishi wote kwa sababu ya wao wenyewe kutofahamu sheria au kusigana kwao na mwandishi mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic