September 30, 2017


Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero amesema sasa anaendelea vizuri baada ya ile ya ajali ya gari jijini Amsterdam nchini Uholanzi.
Aguero alivunjika mbavu baada ya taxi iliyokuwa imewabeba yeye na rafiki yake kuwapeleka uwanja wa ndege kugonga nguzo ya barabarani.

Kutokana na ajali hiyo Aguero raia wa Argentina analazimika kukaa nje ya uwanja angalau wiki nne na anaanza kwa kuukosa mchezo dhidi ya Chelsea, leo.
Lakini mwenyewe amesisitiza kwamba anaendelea vizuri na akatoa shukurani kwa wafanyakazi wa hospitali iliyompokea na kumpatia matibabu.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic