September 3, 2017

Mara baada ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuichabanga Botswana mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki, Jumamosi hii tayari kambi ya Stars imevunjwa.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Salum Mayanga zinaeleza kuwa wachezaji wa timu hiyo wlairuhusiwa kuondoka asubuhi ya Jumapili na wameruhusiwa kurejea kwenye klabu zao.

Imeelezwa kuwa program ijayo itawakutanisha wachezaji hao kwenye kalenda ya Fifa kwa kuwa kwa sasa Stars haishiriki katika michuano yoyote ya kimashindano.

Katika mchezo huo wa kirafiki, mabao ya Stars yaliwekwa wavuni na Simon Msuva ambaye anacheza soka la kulipwa Morocco.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic