Kocha Frank de Boer amefukuzwa kazi ya kuifundisha Crystal Palace ikiwa ni siku 77 tu zimepita tangu alipoteuliwa kuchukua nafasi hiyo.
Hatua hiyo imekuja kutokana na matokeo mabaya katika michezo ya mwanzoni katika Premier League, ambapo sasa nafasi ya kocha huyo inaaminika inaweza kuchukuliwa na Roy Hodgson ambaye ni kocha wa zamani wa England.
Kikosi cha De Boer kimeshindwa kufunga bao wala kupata pointi katika Premier msimu huu, huku kufukuzwa kwake kukimfanya aingie kwenye rekodi ya kuwa mmoja wa makocha aliyedumu muda mfupi zaidi katika Premier League.
Msimu uliopita kocha huyo alifukuzwa kazi katika kikosi cha Inter Milan akiwa amefanya kazi yake hiyo katika siku 85, hivyo mzimu wa kufukuzwa umeendelea kumuandama.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, kocha huyo amewashukuru mashabiki, wachezaji na benchi la ufundi la Palace huku akisema amesikitishwa na kilichotokea.
0 COMMENTS:
Post a Comment