September 15, 2017





Pamoja timu za Simba na Yanga ziko sawa kipointi, lakini kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima ameibuka na kusema kuwa hawatakiwi kulinganishwa na Yanga kwa sasa badala yake mashabiki wanatakiwa kuwapima uwezo wao baada ya kupita michezo mitano ijayo ya ligi kuu.

Niyonzima, raia wa Rwanda, amesema hayo wakati kikosi chao kikilingana pointi na Yanga, wote wakiwa na pointi nne baada ya michezo miwili ya ligi lakini wao wapo juu kutokana na idadi kubwa ya mabao waliyonayo.

Niyonzima keshokutwa Jumapili atakuwa sehemu ya wachezaji wa Simba ambao watashuka dimbani kucheza mchezo wa tatu wa ligi wa timu hiyo dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga, mechi ambayo inatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.  
Mnyarwanda huyo amesema kuwa ni mapema mno kuanza kuwajaji juu ya uwezo wao mbele ya mahasimu zao hao lakini ukweli wa kila kitu utajulikana baada ya kupita kwa mechi hizo tano zijazo za ligi kuu.

“Yanga ni timu nzuri na kila mmoja analijua hilo kwani wamesajili wachezaji ambao wamewaongezea kitu ndani yao na nilishasema tangu zamani kuwa ni timu nzuri na bora, lakini suala la kuanza kutulinganisha nao nadhani hilo kwa sasa mashabiki wanatakiwa waliweke pembeni.


“Nadhani itakuwa vizuri kama tutaanza kulinganishwa na timu zote za ligi kuu baada ya michezo mitano ijayo, ambapo michezo hiyo ndiyo itaamua ni nani yuko vizuri kuliko mwenzake na hapo ndipo itakuwa kipimo bora zaidi kwetu na kwao kuliko ilivyo hivi sasa,” alisema Niyonzima.

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic