September 15, 2017



Mshambuliaji Mnyarwanda, Danny Usengimana, amepona majeraha ya mguu yaliyokuwa yakimsumbua, ambapo amesema anataka kuanza ligi kwa kishindo kuhakikisha anaisaidia timu yake ya Singida United kufanya vizuri msimu huu.

Mnyarwanda huyo amejiunga na Singida United msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Polisi ya Rwanda, kabla ya kutua Singida, alikuwa Mfungaji Bora wa Ligi ya Rwanda kwa misimu miwili mfululizo.

Endapo Usengimana atakuwa na kasi yake ya kufunga mabao kama alivyokuwa Rwanda, basi straika wa Simba, Emmanuel Okwi, atakuwa na kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha anakuwa mfungaji bora msimu huu kutokana na sasa kuongoza akiwa na mabao manne.

“Namshukuru Mungu nimepona majeraha ya mguu yaliyokuwa yakinisumbua, na tayari nimeanza mazoezi kwa ajili ya kuitumikia timu yangu na natarajia kucheza mechi ijayo ya ligi.


“Kazi yangu ni kufunga na nataka niendelee kufunga kama ilivyokuwa kule nilipotoka kwa ajili ya kuisaidia timu yangu kufikia malengo,” alisema Usengimana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic