FULL TIME
Dakika ya 93: Mwamuzi anamaliza mchezo, matokeo ni 0-0, hakuna mbabe.
Dakika ya 92: Presha ni kubwa ikiwa imesalia dakika moja.
Dakika ya 90: Zimeongezwa dakika 3.
Dakika 89: Mashabiki wanaonekana kuwa na presha, timu zote zinacheza kwa tahadhari.
Dakika ya 93: Mwamuzi anamaliza mchezo, matokeo ni 0-0, hakuna mbabe.
Dakika ya 92: Presha ni kubwa ikiwa imesalia dakika moja.
Dakika ya 90: Zimeongezwa dakika 3.
Dakika 89: Mashabiki wanaonekana kuwa na presha, timu zote zinacheza kwa tahadhari.
Dakika ya 87: Simba wanaponea chupuchupu kufungwa baada ya shuti kali kupita pembeni kidogo ya lango.
Dakika ya 81: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Gyan anaingia Mohamed Ibrahim 'Mo'.
Dakika ya 80: Simba wanafika langoni mwa Azam mara mbili mfululizo, lakini walinzi wa Azam wanakuwa makini.
Dakika ya 75: Kasi ya mchezo imepungua kiasi.
Dakika ya 68: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Kichuya, anainfia Said Ndemla.
Dakika ya 67: Mchezo umebalansi kwa timu zote.
Dakika ya 62: Mchezo unaendelea kwa kasi.
Dakika ya 60: Bocco anapiga shuti linadakwa.
Dakika ya 57: Azam wanafanya mashambulizi mawili ya nguvu, lakini Simba wanatulia na kupiga pasi.
Dakika ya 55: Yahaya wa Azam anapiga shuti linapita pembeni kidogo ya lango la Simba.
Dakika ya 50: Simba wanafika langoni mwa Azam lakini wanakosa umakini.
Dakika ya 49: Mbaraka Yusuf wa Azam anacheza faulo.
Kipindi cha pili kimeanza.
MAPUMZIKO
Dakika ya 47: Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza, timu zote zimeenda kupumzika.
Dakika ya 45: Mwamuzi anaonyeshga dakika mbili za nyongeza.
Dakika ya 41: Timu zote zinapokezana kumiliki mpira.
Dakika ya 40: Mchezo umepungua kasi lakini soka la nguvu limetawala.
Dakika ya 35: Yahaya wa Azam anagongwa na Mwanjali wakati wa kuwania mpira hewani, anaumia na kulala chini, anapatiwa matibabu.
Dakika ya 32: Azam wanafanya shambulizi kali, shuti la Yahaya linapanguliwa na Aishi Manula.
Dakika ya 26: Simba wanapata kona, anapiga Kichuya inadakwa na kipa wa Azam.
Dakika ya 24: Nahodha wa Simba, Method Mwanjali yupo chini, mchezo umesimama kwa muda, anapatiwa matibabu ya mguu.
Dakika ya 21: Mchezo ni mkali, umetawaliwa na mbinu nyingi.
Dakika ya 18: Azam wanapiga shuti kali nje ya boksi linadakwa na Aishi Manula.
Dakika ya 13: Azam wanatengeneza nafasi mara kadhaa, mchezo unakuwa na kasi, timu zote zinapiga pasi ndefu.
Dakika ya 10: Nahodha wa Azam, Himid Mao anapewa kadi ya njano kwa kucheza faulo.
Dakika ya 7: Mchezo umeanza kwa kasi, ushindani upo sehemu ya katikati ya uwanja.
Dakika ya 5: Simba wanafanya shambulizi kali, mpira wa kichwa unaokolewa na kipa wa Azam FC inakuwa kona.
Dakika ya 2: John Bocco wa Simba anapuliziwa filimbi kwa kuunawa mpira, analalamika akidai mpira ulimgonga kifuani.
Mchezo umeshaanza dakika ya kwanza.
Timu zote zimeshaingia uwanjani, muda wowote mchezo utaanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment