WAKATI leo kikosi cha Simba kikitarajia kuwavaa Azam, kiungo mchezeshaji wa Simba, Haruna Niyonzima, amefunguka kuwa atatumia uwezo wake kuhakikisha anakisaidia kikosi chake kupata ushindi mbele ya wapinzani wao hao.
Niyonzima leo atawaongoza wenzake wa Simba kucheza na Azam kwenye pambano la Ligi Kuu Bara litakalopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, nje kidogo ya Jiji la Dar. Mara ya mwisho vikosi hivi kukutana Azam waliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Kiungo huyo wa zamani wa Yanga, amesema kuwa yuko vizuri kuhakikisha anaisaidia timu yake mbele ya Azam baada ya kushindwa kumaliza kwenye pambano lao la kwanza mbele ya Ruvu Shooting kufuatia kuumia.
“Niko vizuri kwa ajili ya mechi hii, na naamini nitakuwa sehemu ya msaada mkubwa kwa timu yangu kupata ushindi mbele ya wenzetu Azam, tunaingia kwenye mchezo huu tukiwa na lengo la kuendeleza kupata matokeo mazuri.
“Naamini kwa uwezo wangu itakuwa faida kwa kikosi chetu kupata ushindi na nitajituma kwa hali ya juu ili tu nionyeshe uwezo kwa sababu mechi ile ya kwanza sikuweza kupata nafasi ya kumaliza baada ya kupata majeraha lakini safari hii nataka kuwaonyesha watu uwezo wangu,” alisema Mnyarwanda huyo.

0 COMMENTS:
Post a Comment