September 9, 2017

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ametumia ukurasa wake wa Facebook kuweka picha akiwa na mashabiki jijini Mwanza kisha kuelezea kilichotokea.

“Nyegezi stendi ya mabasi, hapa Mwanza, vijana wameniparamia wakasema hakuna kuondoka bila kubaki na ukumbusho wa picha yangu maana wanaipenda sana Ruvu Shooting!

“Nzuri zaidi wameiombea na kuitabiria ushindi timu yao hii ya Ruvu Shooting dhidi ya Kagera Sugar, kesho, Kaitaba. 

“Rangi za nguo walizovaa wamesema, hazina uhusiano wowote na ushabiki kitimu, ni vazi tu kama mavazi mengine ya kawaida. Wamesisitiza, wao ni Ruvu Shooting!

“Raha sana kuishabikia Ruvu Shooting!”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic