September 1, 2017

Mshambuliaji mkongwe wa Everton, Wayne Rooney amekutwa na tukio lakushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuendesha gari akiwa amelewa.

Tukio hilo lilitokea karibu na nyumbani kwake Cheshire wakati alipokuwa akirejea nyumbani.

Rooney ambaye anaongoza kufunga mabao mengi katika timu ya taifa ya England licha ya kuwa ameshastaafu kuichezea timu hiyo, alikumbwa na tukio hilo jana usiku wakati akitoka kwenye mambo yake binafsi.

Baada ya polisi kumsimamisha na kumpima ilionekana ana kilevi ndani ya mwili wake, hivyo akachukuliwa na kupelekwa kwenye kituo cha pilisi cha karibu kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hakuna taarifa zaidi juu ya tukio hilo. Hadi ana staafu Rooney alifunga mabao 53 katika timu ya taifa kwenye mechi 119 alizocheza. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic