September 14, 2017



Siku moja tu baada ya Mbeya City kuvunja mkataba na kocha wake, Kinnah Phiri raia wa Malawi, baadhi ya wajumbe wa bodi, wameliamsha dude.

Wajumbe hao wameonyesha wazi kutovutiwa na kocha Mohammed Kijuso ambaye amekabidhiwa mikoba.

Wajumbe hao wa bodi ya Mbeya City wametaka timu hiyo kusajili kocha mwenye hadhi ya kikosi.

“Unajua tumekuwa tukilalamika, tumeuambia sana uongozi lakini tunaona kama wanapuuzia. Wenzangu wanakerwa na hiyo hali na wengine wanataka kujiuzulu.

“Mimi sipendi sana kuzungumza lakini nachukizwa na uongozi kutupuuza. Kichuso bado hana hadhi ya kuinoa Mbeya City kama kocha mkuu, tunataka aondolewe,” alieleza mmoja wa wajumbe hao ambaye hakutaka kuandikwa.

Baada ya Mbeya City kuvunja mkataba na Phiri, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla aliwataka kuhakikisha wanamlipa kocha huyo fedha zake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic