October 23, 2017


Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu na yule wa Simba, Ibrahim Ajibu ndiyo wachezaji wa Ligi Kuu Bara wanaozungumzwa zaidi mitandaoni kwa sasa.

Gumzo la Ajibu na Okwi limeshika kasi kubwa kutokana na mambo matatu:

MABAO:
Okwi raia wa Uganda ana mabao 8 wakati Ajibu tayari ametupia matano. Hali ya kasi ya kufukuzana kwao na upinzani wa timu zao umesababisha mjadala mkubwa.

Wako wanaamini Ajibu atamfikia Okwi na wengine wakisema hana nafasi hiyo.

UZURI WA MABAO:
Mjadala wa nani amefunga mabao mazuri zaidi nao umechukua nafasi kubwa, wako wanaosema ni Okwi na wengine Ajibu.

Hali hiyo imekuwa ikisababisha mvutano mkubwa na kila mmoja akiamini tofauti au kuwa kwenye kundi moja.

KUZIBEBA TIMU:
Nani zaidi kaibeba timu, kafunga mabao katika mechi zipi na pointi zilikuwaje nao umekuwa ni mjadala mbadala kutaka kupata uhakika kuwa yupi anaibeba timu zaidi.

Mijadala hiyo haina mwisho kwa kuwa kwa kiasi kikubwa inaonekana kutawaliwa na ushabiki badala ya hali halisi hivyo kuifanya iwe endelevu na hoja mpya kila wakati zikianzishwa.

2 COMMENTS:

  1. ninachofahamu mimi OKWI magoli yote aliyofunga amefungia uwanja wa uhuru tena goli lile lile moja akienda mikoani hakuna anachofanya..tofauti na Ajibu(mguu wa dhahabu) UHURU anafunga na mikoani anafunga pia...aliwafunga ndanda Uhuru..nihayo tu saleh metodo

    ReplyDelete
  2. kuhusu nani kaisaidia timu..AJIBU amefunga magoli matatu yaliyoipa YANGA pointi tisa amefunga goli dhidi ya njombe mji fc, pia akaifunga ndanda fc, pia akawafunga kagera sugar goli la pili...ukiangalia uhalisia ni AJIBU ambaye ametoa mchango mkubwa kwa timu yake kuchukua point hizo 9..

    OKWI , ameisaidia simba kuepuka kipigo kutok kwa MTIBWA hivyo wakaambulia Pointi 1...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic