October 11, 2017



Benchi la ufundi la Yanga limeanza kuingiwa hofu kuwa mshambuliaji wake, Donald Ngoma, raia wa Zimbabwe anaweza kuikosa mechi dhidi ya Simba Oktoba 28.

Hii inatokana na kuandamwa na majeraha mfululizo, hivyo umechukua uamuzi wa kumpumzisha kwa siku saba kuanzia jana kutokana na kuonekana majeraha yake hayajapona vizuri.

Yanga na Simba zitavaana katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara Oktoba 28.

Lakini Yanga itasafiri leo au kesho kwenda Bukoba kuivaa Kagera Sugar, mechi hiyo ya Jumamosi sasa ni uhakika Ngoma ataikosa.

Ngoma alianza kuumwa misuli ya paja hivi karibuni ambapo amelazimika kupewa siku saba kwa ajili ya mapumziko ili kuangalia  afya yake kabla ya kuanza mazoezi mepesi.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema, Ngoma amepewa siku saba za mapumziko kwa ajili ya kuangalia afya yake huku akiwa anaendelea na matibabu ili kuimarika kwa ajili ya kurejea akiwa salama kwa ajili ya mapambano ya ligi.

 “Ngoma amepewa siku saba za mapumziko kwa ajili ya kuangalia afya yake kutokana na tatizo lake la misuli ya paja inayomsumbua akiwa chini ya uangalizi wa daktari ambapo amepewa muda huo tangu juzi," alisema na kusisitiza atakuwa akifanya mazoezi mepesi.

.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic