October 11, 2017


Bosi wa benchi la ufundi la Azam FC, Aristica Cioaba raia wa Romania amesema Mwadui FC si timu ya kuifanya mzaha.

Mwadui FC itaivaa Azam FC katika mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara, wikiendi hii.

Azam inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 11 wikiendi hii itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga kwa ajili ya kucheza na wageni wenyeji wao Mwadui wanaofundishwa na Kocha Jumanne Ntambi.

Mromania huyo amesema wanaenda kwa tahadhari kubwa kwenye mchezo huo wakiogopa kupata matokeo mabaya kutokana na wapinzani wao wengi hasa wa mikoani kukamia wanapokuwa kwao.

“Najua utakuwa mchezo mgumu sana kwa sababu mara nyingi tunapokuwa ugenini ni ngumu sana kupata pointi tatu kwa sababu wanakamia kwa ajili ya kutopoteza kwa sababu wanatambua wakitoka nje wanafungwa kirahisi.


“Kwetu tumeshajiandaa vya kutosha kwa ajili ya mchezo huo na nina uhakika mkubwa wa kushinda kuendeleza rekodi ambayo tumeanza nayo tangu mwanzoni mwa msimu huu, na lengo letu kubwa ni kumaliza kwenye nafasi tatu za juu,” alisema kocha huyo. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic