October 22, 2017



FULL TIME
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 90, Stand wanapata mpira nje ya eneo la 18, mpigaji anapaisha juuuuu
Dk 87, mpira wa kona, Tshishimbi anaunganisha vizuri hapa, kipa anaokoa na kuwa kona. Inachongwa Stand wanaokoa
SUB Dk 82 Emmanuel Martin anaingia kuchukua nafasi ya Mwashiuya
Dk 80, hakuna dalili za Stand kusawazisha, hakuna presha kubwa langini mwa Yanga na hali ilivyo Stand wanaweza kufungwa tena
Dk 77, Stand wanapata kona, mpira wa Kibopile, Rostande anaruka vizuri na kudaka
SUB Dk 77 Chirwa anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Yussuf Mhilu
Dk 76, Mussa anaunganisha krosi ndani ya lango la Stand, kidogo unatoka nje


SUB Dk 74, Muhonge anakwenda anakwenda benchi na anaonekana kwenda kwenda moja kwa moja 
SUB Dk 70 Ajibu anakwenda nje na Said Mussa anaingia kuchukua nafasi yake
GOOOOOOOO Dk 69, Chirwa anaindikia Yanga bao la nne baada ya uzembe wa kipa Muhonge kutoka mapema langoni halafu akaukosa mpira
SUB Dk 67 Mahela anaingia kuchukua nafasi ya James upande wa Stand
Dk 63 Shambulizi jngine la Yanga hapa, wanapata kona. Hata hivyo Ajibu anaichonga kwa mbwembwe inaokolewa
Dk 61 Muhonge anatoka langoni mwake kuokoa, anapigwa chenga na Chirwa anayeingiza mpira mzuri ndani ya 18 lakini Tshishimbi anaukosa, Stand wanaokoa
Dk 60, Rostande anafanya kazi ya ziada na kuokoa vizuri
Dk 60, Salamba anamtoka Kessy, hata hivyo anajitahi na kuutoa, kona. Inachongwa na Aaron, inakuwa kona tena
Dk 57, Stand wanapata kona nyingine, Kibopile anachonga kona, Yanga wanaongosha
 Dk 56, Ajibu anamtoka beki wa Stand hapa, krosi safi kabisa lakini Muhonge anafanya kazi ya ziada na kuokoa


Dk 54, Rostande anaruka na kuokoa kona ambayo Stand wamepiga, Cannavaro anaondosha
GOOOOOOOOO DK 53, Buswita anafunga bao safi kabisa akiunganisha mpira wa kona
Dk 52, Yanga wanapata kona nyingine baada ya Ajibu kutaka kuwatoka mabeki wa Stand
Dk 50, Muhonge anaruka na kudaka vizuri kabisa mpira wa kona ya Mwashiuya
Dk 49, Yanga wanagongeana vizuri kabisa, mpira wa shuti la Ajibu unaguswa na kuwa kona
KADI Dk 46 Kibopile analambwa kadi ya njano kwa kuchelewesha mpira
Dk 45 Mpira unaanza kwa kasi Stand wakionekana wamepania kusawazisha


MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, Stand wanafanya shambulizi jingine lakini shuti la Salamba linamgonga mwenzake
SUB Dk 43 Bakari Mohamed anaingia kuchukua nafasi ya Kitoba
Dk 41, Muhonge analazimika kuokoa mpira mwingine wa kona, kona tena, inachongwa na Mwashiuya, Stand wanaondosha
Dk 40,  Yanga wanapata kona baada ya shambulizi, kipa Muhonge anafanya kazi ya ziada kukoa kona tena
Dk 34, Stand wanapata kona ya kwanza kupitia mpira wa kurusha, inachongwa lakini Rostande yuko vizuri...
GOOOOOOOO Dk 30 katikati ya mabeki wa Stand, pasi nzuri ya Chirwa, Ajibu anaachia mkwaju mkali kabisa na kuandika bao la pili


Dk 29, Yanga inapata kona, inachongwa, Stand wanaokoa na kuwa kona tena. Anachonga tena Ajibu, Cannavaro anapiga kichwa, kipa anawahi
Dk 26, Ajibu tena anajaribu akiwa karibu kabisa, Muhonge anaw
GOOOOOOOOO Dk 24, Ajibu anafunga bao zuri kabisa la mpira wa adhabu akimuacha Muhonge
Dk 21 Ajibu anajaribu tena kwa mkwaju wa adhabu lakini inaonekana halikuwa shuti kali
KADI Dk 19, John Mwitiko analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Tshishimbi
Dk 18 Salamba anaingia vizuri kabisa, lakini shuti lake linakuwa nyanya kwa Rostande
Dk 17, Stand wanapata nafasi ya mkwaju wa adhabu, lakini mpigaji anapaisha juuuu
Dk 14, Cannavaro analala na kuokoa wakati Stand wakienda kushambulia, mashabiki wanamshangilia 


Dk 13, Rostande analazimika kuruka juu na kuokoa mpira wa krosi lakini Stand nao wanaonekana hawajipangi vizuri wanaposhambulia
Dk ya 10 sasa, Yanga wanaonekana kuutawala mpira huku kukiwa hakuna mashambulizi kutoka kwa Stand na kama Stand wataacha Yanga waendelee kufanya hivi ni rahisi sana kufungwa
Dk 7, Yanga wanagongeana vizuri lakini Stand wanaonekana wako vizuri katika mipira ya juu
Dk 5, mkwaju matata wa faulo wa Ajibu, kipa Muhonge anaokoa vizuri kabisa
Dk 2, Yanga wanapata kona baada ya mabeki wa Stand kuutoa mpira. Inachongwa lakini Stand wanaokoa vizuri kabisa
Dk 1, faulo nzuri ya Hamad Kibopile, mpira unamtoka Youthe Rostand lakini anajitahidi kuuwahi
Dk ya 1, mechi ndiyo inaanza na Yanga wanafanya madhambi nje kidogo ya 18

1 COMMENTS:

  1. Yanga wamekuwa watete hata vivuli vyao wanafikiri akina Okwe naKichuya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic