October 21, 2017



Ili kuhakikisha anaimarisha safu yake ya ushambuliaji, Kocha Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina ameanza kuwasuka upya washambuliaji, Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa.

Hiyo imetokea siku chache wakiwa wametoka kushinda mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. Mabao ya Yanga yalifungwa na Ajibu na Chirwa.

Mzambia huyo, amefikia hatua hiyo ya kuwasuka nyota hao baada ya Donald Ngoma kutopona haraka majeraha ya nyama za paja na huenda akawa nje ya uwanja kwa muda mrefu.


Kutoka katika benchi la ufundi la Yanga, mmoja wa wahusika amesema Lwandamina ameanza kutengeneza kombinesheni itakayoelewana na kucheza muda mrefu ya Ajibu na Chirwa wakati Ngoma akiwa anauguza majeraha yake.

Mtoa taarifa huyo alisema, kocha huyo amemhamisha Chirwa kucheza namba tisa nafasi iliyokuwa inachezwa na Ngoma. Zamani Chirwa alikuwa akicheza pembeni.

“Benchi la ufundi limefurahishwa na uchezaji mzuri wa ushirikiano wao kwa maana ya kombinesheni iliyocheza kwa kuelewana kwa muda mfupi na kufanikiwa kupata ushindi katika mechi iliyopita na Kagera.

“Kama unavyojua tangu ligi imeanza Ajibu na Chirwa hawakuwahi kucheza pamoja namba tisa na kumi, lakini mechi dhidi ya Kagera walicheza kwa mara ya kwanza na wakafanya vizuri na kila mmoja akafunga,” kilisema
chanzo chetu.

Alipotafutwa Lwandamina alisema: “Nataka kila mchezaji awe na uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja na hiyo ndiyo falsafa yangu, ninafurahia kuona ushirikiano mzuri wa Ajibu na Chirwa."

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic