October 21, 2017




Kiungo anayekuja kwa kasi, Mohammed Issa ‘Banka’ wa Mtibwa Sugar, amesema yupo tayari kuichezea timu yoyote ile itakayomuhitaji katika usajili wa dirisha dogo mwezi ujao, iwe Yanga au Simba, yeye anaangalia fedha tu.

Banka anayefan-anishwa kiuchezaji na kiungo wa zamani wa Yanga na Simba, Mohammed Banka amesema kati ya Simba au Yanga pengine hata timu nje ya hizo anaweza kujiunga nazo endapo fedha itakuwepo.

Kiungo huyo amekuwa akiisaidia kwa kiwango kikubwa timu yake katika mechi kadhaa, huku akiwa miongoni mwa wachezaji waliozipa ugumu Simba na Yanga walipokutana nazo hivi karibuni.

Kiungo huyo alisema yupo tayari kusajiliwa na mojawapo ya timu hizo mara baada ya makubaliano ya kimkataba kwani lengo lake kubwa ni kuona anafika mbali.

“Nahitaji kufika mbali katika maisha yangu ya soka ikiwezekana kujituma ipasavyo kuweza kufanikiwa kama ilivyo kwa Mbwana Samatta.

“Iwapo Simba na Yanga zitanihitaji kunisajili nitakuwa tayari kuzichezea kwa kuwa moja ya malengo yangu ni kufanikiwa katika soka na hata kuichezea timu mojawapo kati ya hizo,” alisema Banka.

Mtibwa Sugar imekuwa timu inayotengeneza wachezaji na kuwa na viwango vinavyokubalika ambapo baadaye Simba, Yanga na Azam FC zinawasajili na kuwatumia kwa mafanikio.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic