October 13, 2017



Kagera Sugar ina uhakika itapambana kwa kila njia kuhakikisha Yanga inaacha pointi zote tatu kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kesho.

Kikosi cha Kagera Sugar kitakuwa wenyeji wa Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba jijini Dar es Salaam, kesho.

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Meck Maxime amesema kikosi kipo vizuri na wamejiandaa vya kutosha.

“Tumejiandaa kufanya vizuri na mashabiki waje tu, wachezaji wako tayari na watawapa kile wanachotaka,” alisema.


Pamoja na kuwa na mwendo wa kusuasua katika Ligi Kuu Bara, Maxime anaamini maandalizi ya kikosi chake ni mazuri na wataifunga Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic