Azam FC wametoa sababu tatu wanazoamini kesho wana nafasi ya kuishinda Mwadui FC kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Iddi Cheche maarufu kama Bab Cheche, amesema kikosi chao kiko tayari kwa ajili ya mechi hiyo ya kesho ugenini.
Lakini akasema uwanja wa Mwadui una nyasi bora kabisa kwa ajili ya kuchezea mpira ambayo ni sababu ya kwanza.
"Pili ni hali ya hewa inaruhusu kabisa na tunaamini tutacheza vizuri na mwisho ni sisi tuko vizuri," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment