Yanga imeingia kwenye hofu ya kutaka inaingia katika mechi yake ya Oktoba 28 dhidi ya watani wake Simba bila kuwakosa wachezaji muhimu.
Hofu inatokana na kadi za njano ambazo wachezaji wake muhimu kama Kelvin Yondani, Juma Abdul na Raphael Daud kuwa na kadi mbili za njano.
Wote watatu walipata kadi ya pili katika mechi iliyopita Yanga ikiigaragaza Kagera Sugar kwao Kaitaba kwa mabao 2-1.
Hali hiyo inawafanya Yanga kuwa makini zaidi kabla ya mechi itakayofuata dhidi ya Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment