Kiungo mchezeshaji wa Simba Mnyarwanda, Haruna Niyonzima ametamka kuwa ipo siku kiungo Mghana, Nicholas Gyan atakubalika Msimbazi.
Kauli hiyo, aliitoa hivi karibuni baada ya baadhi ya mashabiki kubeza kiwango cha Mghana huyo aliyejiunga na timu hiyo kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara akitokea Ebusua Dwarfs ya nchini Ghana.
Niyonzima alisema kiungo huyo kilichompata sawa na yeye alichokipata tangu ajiunge na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika, mwakani.
Niyonzima alisema kiungo huyo hakuwa na maandalizi ya kutosha ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu kwa maana ya kambi ya pamoja waliyoweka wachezaji wengine Afrika Kusini.
“Nikwambie kitu kimoja, kitu cha kwanza kinachofanya Gyan asionekane bora hakitofautiani na mimi, kama unakumbuka mimi na yeye tulijiunga na timu pamoja wakati wenzetu wametoka kambini Afrika Kusini.
“Hivyo, utaona kabisa tumekosa maandalizi ya pamoja ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu kwa kukosa mazoezi na ndiyo kitu kinachonitesa mimi na Gyan.
“Nikwambie kitu, ipo siku mashabiki wa Simba watamkubali na kitu ambacho anachotakiwa kukifanya ni kuachana na presha ya mashabiki akiwa uwanjani na badala yake kufanya kazi yake pekee,” alisema Niyonzima.
0 COMMENTS:
Post a Comment