October 16, 2017




Clifford Marion Ndimbo ndiye atakuwa msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Taarifa kutoka ndani ya TFF zinaeleza, Ndimbo ameanza kazi leo rasmi.

“Ndimbo ameanza kazi leo na atashirikiana na Alfred Lucan katika majukumu katika kitengo cha usemaji,” kilieleza chanzo.

"Unajua kitengo cha habari cha TFF sasa kimetanuka kwa kiwango kikubwa. Kuna usemaji na masuala mengine kama mitandaoni na kadhalika. Hivyo hawa mabwana inabidi wasaidiane."


Ndimbo aliwahi kuwa msemaji wa Simba lakini ni mtangazaji mkongwe ambaye mara ya mwisho alisikika akiwa na Times FM.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic