October 2, 2017



Kocha Mkuu wa Singida United, Hans van Der Pluijm, ameweka bayana kuwa bahati pekee ndiyo iliyosababisha wapinzani wao Azam waambulie sare mbele yao wakati walipovaana juzi Jumamosi katika mchezo wa ligi kuu.

Pluijm, raia wa Uholanzi, juzi aliiongoza Singida United kupambana na Azam kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao uliisha kwa sare ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Bao la Singida United lilifungwa na Mnyarwanda, Danny Usengimana, wakati la Azam lilifungwa na Peter Paul.

Mholanzi huyo amesema waliwabana wapinzani wao kuhakikisha hawapati bao kwenye mchezo huo lakini makosa madogo waliyoyafanya kwenye dakika za mwisho, ndiyo ambayo yaliwaokoa wapinzani wao.
“Tulicheza vizuri na tuliwabana vyema wapinzani wetu kwamba wasipate pointi kwetu wala bao na hilo tulilifanikisha kwa dakika nyingi kabla ya mwisho kabisa kufanya makosa kidogo ambayo yaliwapa bao la kusawazisha.
 “Lakini kingine ambacho kiliwafanya wenzetu waambulie pointi moja ni bahati waliyokuwa nayo ya kupata bao hilo ambalo hata ukiangalia lilikuwa la piga nikupige langoni mwetu, lakini ukija kwenye suala la kiwango sisi tulicheza vyema kuliko hata wao,” alisema Mholanzi huyo.

SOURCE: CHAMPIONI   


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic