October 2, 2017



Mkongwe katika kiungo cha Mtibwa Sugar, Shaaban Nditi, amewaambia Yanga washukuru suluhu waliyoipata, kwani walikuwa wanakufa.

Yanga ilivaana na Mtibwa juzi Jumamosi katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Hiyo ni sare ya tatu kwa Yanga kwenye mechi tano za Ligi Kuu Bara walizocheza, nyingine ni dhidi ya Lipuli FC na Majimaji.

 Nditi amesema katika mechi hiyo walikuwa na matumaini makubwa ya kuifunga Yanga kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

"Suluhu hii tuliyoipata imetuvurugia mipango yetu, kwani katika mechi hiyo tuliingia uwanjani kwa lengo moja la kuchukua pointi tatu ili tuendelee kukaa kileleni.

"Lakini hayo yote ni matokeo na tunajipanga kwa ajili ya mechi nyingine zinazofuata za ligi kuu ili kuhakikisha tunashinda ili tusitoke kileleni," alisema Nditi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic