October 17, 2017


Kulia kocha wa timu ya Singida United Hans Van der Plujim na Nahowa wa timu hiyo wakikabidhi jezi iliosainiwa na wachezaji kwa Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji, Mr Tarimba Abbas.



Singida United wanaoshiriki Ligi Kuu Bara wamefanya ziara katika ofisi za wadhamini wao Sportpesa na kuwakabidhi zawadi ya jezi yenye saini za wachezaji na makocha wa kikosi hicho.

Ziara hiyo imefanyika jana mchana wakati wachezaji hao walipokwenda kwenye ofisi za Sportpesa ambao ni wadhamini wao wakuu.

Kikosi cha Singida United, kimetua katika makao makuu ya wadhamini wake kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.

Wachezaji, makocha na viongozi wa Singida United wakiongozwa na Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm wametua katika ofisi hizo zilizopo Oysterbay jijini Dar es Salaam kufanya ziara fupi.


Singida United wanakuwa wa pili kufanya ziara katika ofisi za SportPesa baada ya Simba ambao walifanya hivyo wiki iliyopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic