Ingawa bado inaonekana ni mbali lakini presha ya pambano la watani Yanga na Simba imeanza.
Mechi itapigwa Oktoba 28, mwaka huu kikosi cha Yanga kitashuka uwanjani kupambana na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, mshambuliaji wa Yanga raia wa Burundi, Amissi Tambwe, amesema kuwa anaitamani mechi hiyo na endapo atapata nafasi ya kuanza, basi atafanya makubwa.
Tambwe ambaye alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti yaliyomfanya mpaka sasa ashindwe kuitumikia Yanga katika mchezo wowote ule, alisema ana hamu kubwa sana ya kucheza mechi hiyo ili aweze kuiendeleza rekodi yake ya kuifunga Simba mara kwa mara.
“Namshukuru Mungu hivi sasa nipo fiti na ninaendelea vizuri ila natamani sana kuitumikia timu yangu katika mchezo dhidi ya Simba.
“Mpaka sasa sijacheza mechi yoyote ile tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu ila nitafurahi sana kama nitacheza dhidi ya Simba kwani ninaitamani sana mechi hiyo, namuomba Mungu anisaidie ili niweze kuwa fiti,” alisema Tambwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment