October 14, 2017






Ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar umeifanya Yanga kuindoa Simba kileleni mwa Ligi Kuu Bara.

Simba ilikuwa inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 11, lakini ushindi wa leo, Yanga imefikisha pointi 12 sawa na Azam FC iliyoko katika nafasi ya pili baada ya sare ya 1-1 leo dhidi ya Mwadui FC.

Wakati mabingwa hao watetezi wanatua kileleni mwa Ligi Kuu Bara na kuongeza utamu wa ushindani, watani wao Simba watakuwa na kazi kesho dhidi ya Mtibwa Sugar wakitaka kurejea kileleni.

Mechi kati ya Simba dhidi ya Mtibwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam inasubiriwa kwa hamu kubwa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic