February 24, 2021


LICHA ya kuwa sababu ya penalti kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliowakutanisha Yanga na Simba, Uwanja wa Mkapa, Tuisila Kisinda ameambiwa hawezi kupata namba ndani ya Simba.

Manara ameongeza kuwa anaamini kuwa kwa namna ambavyo anafanya ndani ya uwanja akiwa mwanariadha kama ilivyo kwa Filbert Bayi anaweza kutusua.

Penalti hiyo ilizua utata ila mwisho wa siku maamuzi ya mwamuzi hayakuweza kuzuiwa.

Kisinda ambaye anacheza Yanga alisababisha penalti baada ya kumzidi spidi beki kisiki wa Simba, Joash Onyango, Uwanja wa Mkapa wakati Yanga ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1.

Penalti hiyo ilifungwa na Michael Sarpong ilimshinda mlinda mlango namba moja wa Simba Aishi Manula na kuiokotea nyavuni.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa anatambua kwamba Kisinda ni mchezaji makini ndani ya Yanga ila hawezi kupata nafasi ndani ya kikosi cha Simba.

"Unazungumza kuhusu Kisinda,(Tuisila) kuja kucheza Simba? Sasa pale atacheza nafasi ya nani maana kila mtu ana namba yake sijui atamchomoa nani kikosi cha kwanza.

"Labda atapendeza akiwa kwenye masuala ya riadha kama akina Bayi,(Filbert) huko anaweza kufanya vizuri ila ndani ya Simba hakuna nafasi kwa kweli na huo ni ukweli kabisa.

"Unapozungumzia Simba unazungumzia timu moja ambayo kupata namba lazima ukomae na uwe bora ndani ya uwanja sasa na wachezaji ambao wanasajiliwa ni lazima wawe imara na bora," amesema.


Video na mahojiano zaidi tembelea Global TV Online

11 COMMENTS:

  1. Sio penati ya utata ile ni penati ya mwamuzi sababu tukio lilikuwa nje ya uwanja

    ReplyDelete
  2. NA KWELI, MAANA WATU WANAONGEA SANA KUHUSU TK MASTER, SIJAJUA USAJILI WA 2021/22 NANI ATAONDOKA NANI ATABAKI..............NAMUONA AJIBU HUYOOOOOOOOOOOOOOOOOO!

    ReplyDelete
  3. Ajibu haendi kokote, mtamwona sana kwenye kombe la FA...

    ReplyDelete
  4. Replies
    1. Wamiliki wa hii blog wamekuwa hawajali kuwadhibiti wapuuzi kama wewe katika suala la maudhui matokeo yake ndo kama haya
      Ipo siku TCRA watawalipisha faini ya kutosha ndo mtakapoelewa kwa nini tunasisitiza kudeal na watu kama hawa

      Delete
  5. Ila tukubali Manara na wanaomshabikia mnatia huruma upande wa akili .

    ReplyDelete
  6. disrespectful kwa kweli. nje na ushabiki lazima tuheshimu kazi na kipaji cha mtu

    ReplyDelete
  7. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic