October 1, 2017



Maandamano makubwa ya watu wakitaka kupiga kura kujitenga na Hispania hasa wale wanaounga mkono Catalania, yamesababisha FC Barcelona kucheza bila mashabiki.

FC Barcelona imeifunga La Palmas kwa mabao 3-0 katika mechi ya La Liga ambayo imechezwa bila ya mashabiki baada ya polisi kupambana na waandamanaji na watu zaidi ya 450 kuumia.

Beki wa FC Barcelona, Gerard Pique huku akiangua machozi mbele ya waandishi wa habari, ameonyesha waziwazi kupinga polisi kuwapiga mashabiki, huku akisema haikuwa sawasawa hata kidogo.


Pique ambaye anaunga mkono wananchi hao kupiga kura amesema haikuwa sahihi na alicheza mechi hiyo akiomba dakika 90 ziishe haraka kwa kuwa lilikuwa jambo gumu katika maisha yake ya mpira kucheza bila ya mashabiki.

Rundo la mashabiki walikuwa wamezuiwa nje ya Uwanja wa Camp Nou kwa sababu za kiusalama na kulikuwa kuna mjadala mkubwa kama mechi hiyo ichezwe au kusogezwa mbele na Barcalona walielezwa mechi ikiahirishwa, wangepokwa pointi tatu.














0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic