November 13, 2017




Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog ameweka wazi kuwa hali inayomkuta mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi kutofunga wakiwa wanacheza viwanja vya mikoani siyo tatizo kwani kwao haijalishi nani atafunga ila muhimu wapate pointi tatu ambazo zitawafanya waendelee kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi.

Licha ya kufunga mabao nane hadi sasa kwenye ligi Okwi hajafanikiwa kufunga hata bao moja wakati kikosi hicho kikiwa kinacheza kwenye viwanja vya mikoani. Hadi sasa Simba wamecheza jumla ya mechi tatu ambazo zote hizo Okwi hajafunga hata mechi moja.

Omog amesema kuwa hakuna tatizo lolote kwa Okwi kutofunga bao kwenye michezo hiyo kwa sababu yeye anawafundisha washambuliaji wote wa kikosi hicho kuisaidia timu iweze kupata matokeo mazuri kwenye kila mchezo wao.

“Hakuna tatizo kama mchezaji fulani ameshindwa kufunga kwenye mechi zetu moja au mbili za mkoani kisha wengine wakafanikiwa kufunga, siyo vibaya kwamba eti Okwi ameshindwa kufunga basi iwe tatizo.

“Unajua tunachofanya ni kuipigania timu iweze kupata matokeo mazuri katika kila mchezo wetu, inapotokea fulani hajafunga na mwingine amefunga na tumepata ushindi hilo linakuwa jambo bora zaidi kuliko angefunga Okwi kisha timu ikapata matokeo mabaya, hilo lisingekuwa sawa.


“Kama kufunga itatokea atafunga tu kwani mechi zetu nyingi amekuwa anapambana vizuri na utaona hata asipofunga basi atatoa pasi kwa mfungaji na mambo mengine, kwa hiyo kwetu benchi la ufundi wala hatuoni shida kwake,” alisema kocha huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic