November 13, 2017



Unaweza kusema mambo bado tofauti na wengi walivyoamini kuhusiana na mshambuliaji Amissi Tambwe na kiungo Thabani Kamusoko.

Awali ilielezwa, Kamusoko na Tambwe ambao ni majeruhi wangeanza mazoezi leo wakati Yanga ikirejea mazoezini na kuanza na yale ya gym.

Lakini hadi wanamaliza mazoezi, Tambwe na Kamusoko hawakuwa wametokea hali inayoonyesha bado hawajawa tayari kuanza mazoezi na wenzao.

Kamusoko na Tambwe wamekuwa majeruhi kwa muda mrefu ingawa Tambwe raia wa Burundi ndiye amekaa nje kwa muda mrefu zaidi kwani tokea kuanza kwa msimu wa 2017-18, hajaichezea Yanga hata mechi moja.

Hata hivyo, taarifa za kwamba wanatarajia kurejea mazoezini hivi karibuni zimekuwa zikizungumzwa mara kwa mara na kujenga matumaini kwa Wanayanga huenda wakaanza mazoezi hivi karibuni.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic