November 24, 2017


Mahakama ya Italia, imemhukumu Kiungo mshambuliaji wa zamani wa AC Milan, Robinho de Souza kwenda jela miaka tisa baada ya kupatikana na hatia ya kosa la ubakaji.

Robinho amepatikana na hatia ya ubakaji ya dada wa miaka 22, wakati huo akiwa anaitumikia AC Milan.

Hukumu hiyo imetolewa mbele ya wanasheria wake pamoja na watuhumiwa wengine walioshitakiwa na Robinho ambao walielezwa kushirikiana kumbaka dada huyo raia wa Albania wakati huo akiwa na miaka 22.


Hata hivyo, Robinho aliyewahi kuichezea Real Madrid na Manchester City hatarudishwa Italia kwa kifungo hadi hapo atakapokata rufaa au la.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic