Kocha Mkuu wa Manchester United, Jose Mourinho anaamini wachezaji Zlatan Ibrahimovic na Romelu Lukaku wanaweza kuanza wote.
Mourinho amesema Zlatan na Lukaku watapata nafasi ya kuanza na wataonyesha maajabu.
“Watawashangaza wengi, watacheza pamoja na mtashangaza sana,” anasema Mourinho.
Baada ya Zlatan kurejea Manchester United kumekuwa na maswali mengi kuhusiana na namba tisa.
Lakini inaonekana Mourinho amejipanga kuona timu anawatumia washambulizi hao.
Maana yake, mmoja atacheza namba kumi na mwingine tisa na anataka hivyo ili Zlatan amsaidie Lukaku kufunga au yeye amtumie Lukaku kufunga.
0 COMMENTS:
Post a Comment