Kocha mpya wa AC Milan, Gennaro Gatuso amezua gumzo kubwa huku mambo mengi yakizungumzwa.
Baada ya Milan kumtimua kocha wake na kuelezwa Gatuso ndiye atakuwa kocha mkuu, limekuwa gumzo kila upande wakijadili.
Mashabiki wa AC Milan wana hamu ya kuona ataifanyaje hiyo kazi, lakini wako wanaamini hawezi.
Baadhi wamekuwa wakikumbushia tukio lake la kumkaba Kocha wa Tottenham wakati huo, Joe Jordan.
Hivyo gumzo ni hofu kama kweli Gattuso maarufu kama Ringhio anaweza kuwa ni mtu mwenye subira na uvumilivu kama ambavyo makocha wanatakiwa kuwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment