November 17, 2017


Simba itakuwa na kazi ya kuhakikisha inaondoka na pointi tatu ili kupata zote sita mkoani Mbeya.

Kazi hiyo itakuwa Jumapili itakapokutana na wabishi Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.


Kikosi cha Simba, kimeendelea na mazoezi mjini humo kuhakikisha kinakuwa sawa katika mechi hiyo.

Mara ya mwisho, Simba ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City na kupata pointi tatu.


Baada ya hapo, Simba ilibaki katika ukanda huo baada ya kwenda Katavi na baadaye Sumbawanga ambako ilicheza mechi za kirafiki kama sehemu ya maandalizi ya mchezo huo.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic