Mshambuliaji nyota wa Yanga, Amissi Tambwe ameungana na wenzake lakini ameendelea kujifua peke yake.
Tayari Tambwe amehakikishiwa kwamba hatakuwa fiti kuivaa Mbeya City, Jumamosi. Lakini ametakiwa kuendelea kujifua.
“Naendelea kufanya mazoezi lakini natakiwa kufanya taratibu,” alisema.
Wakati wenzake wamekuwa wakiendelea na mazoezi, Tambwe amekuwa akiuzunguka uwanja taratibu.
Hadi Yanga imefikisha mechi 9 za Ligi Kuu Bara, Tambwe hajacheza hata mechi moja.







0 COMMENTS:
Post a Comment