Benki ya TPB imeingia kwenye makubaliano rasmi na Kampuni ya MultiChoice ambapo wafanyakazi, wateja na hata wale wasio wateja sasa wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na kisha kulipia kidogokidogo.
Akizungumza wakati wa kutangaza rasmi makubaliano hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, alisema benki yake siku zote imekuwa ikijitahidi kubuni huduma mbalimbali kwa ajili ya kuwafanya Watanzania wengi zaidi waweze kupata huduma muhimu.
“Benki yetu ni benki ya Watanzania wa kada zote, na wenzetu wa MultiChoice nao hali kadhalika, sasa tumeamua tuungane ili tuwawezeshe ndugu zetu Watanzania kupata fursa ya kuwa na huduma ya DStv kwa njia ambayo ni rahisi kwao,” alisema Moshingi.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, Maharage Chande alisema MultiChoice imekuwa wakati wote ikiwasikiliza wateja Watanzania na kuhakikisha inawafikishia huduma zake kwa njia rahisi zaidi.
Mkopo huo wa kupata king’amuzi cha DStv, umeshaanza na ili kuhakikisha Watanzania wengi wananufaika, vigezo na masharti vilivyowekwa vimezingatia hali halisi ya Watanzania wengi.
0 COMMENTS:
Post a Comment