November 24, 2017



Timu ya Yanga, kesho Jumamosi itashuka uwanjani kupambana na Prisons ya jijini Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.


Hata hivyo, mshambuliaji wa Prisons, Mohammed Rashid amesema wamefurahia mechi yao hiyo kufanyika kwenye uwanja huo, hivyo wanaamini kuwa kama watajituma zaidi basi wanaweza kupata matokeo mazuri kwenye mechi hiyo.


Alisema uwanja huo ni mdogo tofauti na ulivyo ule wa Uhuru na Taifa kwa hiyo wakijipanga vizuri itakuwa ni rahisi kwao kuizuia Yanga kutengeza nafasi za kufunga.

“Tumefurahi mechi yetu na Yanga kufanyika Chamazi, itakuwa ni rahisi kwetu kuwazuia Yanga ukilinganisha na mechi ambazo zinachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru au Taifa.

“Timu nyingi za kutoka mikaoni zimekuwa zikipata wakati mgumu katika viwanja hivyo kwa sababu ni vikubwa lakini kwa huu wa Chamazi tutakuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia lakini pia tutakuwa na uwezo mkubwa wa kulifikia lango la Yanga kwa wepesi zaidi,” alisema Rashid.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic