November 28, 2017

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kasim Majaliwa jana alikabidhiwa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 50 na Mjumbe wa Baraza la wawakilishi, Mohammed Razar kutoka visiwani  Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar.

Razar amekabidhi vifaa hivyo vikiwemo mpira jezi na zawadi za makombe kwa lengo la kuanzishwa mashindano maalum katika majimbo ya mkoa Dar kupitia Chama cha Mapinduzi.

Akizungumza na katika makabidhiano ya vifaa hivyo leo Jumanne, Razar alisema kuwa wamekuwa wakitoa vifaa hivyo kwa lengo la kufanyika mashindano hayo kama ilivyokuwa Unguja na Pemba kwa wanachama wa chama hicho katika kukuza mchezo wa mpira wa miguu nchini.

“Haya tunayafanya hapa, tayari tumeshafanya Unguja na Pemba  na hii kwa hapa Dar tutakuwa ni kwa majimbo 10, lengo lilikuwa ni kukuza mchezo wa mpira wa miguu na pia kutoa ajira kwa vijana ambao wanaweza kuchukuliwa na timu kubwa za hapa, mashindano yatakayoanzisha tunaomba yafuate sheria za FIFA.


  Kwa upande wa waziri mkuu alisema kuwa: “Kwanza washukuru kwa kuweza kutupa vifaa hivi ambavyo  naamini vitaleta tija kwa mashindano yatakayoanzishwa kwa sababu michezo ni ajira lakini inapunguza vijana kukaa vijiweni bila ya kufanya kazi.

“Napokea vifaa hivi na zawadi zake kwa ajili ya hiyo michuano na mimi namkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mashindano hayo ambayo nitapenda yakifanyika kwa haraka pia nitoe rai ya  sheria za Fifa zifuatwe kama walivyoomba wenzetu,” alisema Majaliwa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic