TIMU ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, leo asubuhi ikiwa chini ya Kocha Ammy Ninje ilianza mazoezi kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji inayotarajia kuanza Desemba 3, mwaka huu nchini Kenya ambapo ameanza kwa kufundisha mbinu mbalimbali za kushambulia.
Kilimanjaro ipo kundi moja na Zanzibar Heroes katika michuano hiyo ikiwa pamoja na Libya, Rwanda na Kenya.
Katika mazoezi hayo kocha huyo alitumia muda mwingi kuwaelekeza wachezaji wake namna ya kuweza kushambulia pamoja na kupiga pasi za mwisho ambapo alionekana kuwa makini kwa wachezaji kuhakikisha wanashika mbinu hizo kabla ya kuondoka nchini keshokutwa Alhamisi.
0 COMMENTS:
Post a Comment